
Mwanasoka na kocha maarufu nchini Argentina ambaye pia ni mdogo wake na aloyekuwa mkongwe wa soka nchini humo na dunia nzima, marehemu Diego Maradona, Hugo Maradona (52) amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo jijini Naples.
Hugo alikutwa nyumbani kwake jana Desemba 27 akiwa amekufa. Kifo chake kimetokea ikiwa umepita mwaka mmoja tangu kifo cha kaka yake, Maradona.