
OFISA Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa mapokezi mazuri waliomuonyesha mara baada ya kutangazwa kuitumikia klabu hiyo jana, Jumatatu, Desemba 4, 2022.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Ahmed Ally ameandika; “Msemaji wa Mabingwa nimeamka salama Al hamdullillah🙏🙏
“Awali ya yote nisema asante Wana Simba kwa mapokezi makubwa niliyopata kutoka kwenu hii ni ishara kuwa mnanipenda, mnaniamini na mmenikubali nami niwahakikishie tuu sintawaangusha
“Mapokezi yenu yamenipa nguvu, faraja na matumaini ya kuwa niko sehemu sahihi na sehemu salama, sehemu ya watu wenye upendo wa hali ya juu hakika hii sio timu hii ni Familia,” Ofisa Habari wa Simba SC.