
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hivi karibuni atafanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa.
Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu.
Akizungumzia kuhusu mijadala inayoendelea juu ya serikali yake kukopa kopa, Rais Samia amesema hizo kelele ni Presha ‘Stres’ za kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
“Nataka niwaambie nitatoa list (orodha) mpya ya Mawaziri hivi karibuni, wale wanaotaka kwenda na mimi nitaenda nao ila wale wanaotumika nitawapa nafasi wakatumike huko nje wanapopataka. Wale ninaohisi wanaweza kwenda na mimi…nitakwenda nao.
“Uongozi huletwa na Mungu, aliyepangiwa ndiye atakayekaa. Lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule, na wanafanya kazi kwa ajili ya kule, nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje,” amesema Rais Samia.