×

Rooney Atajwa Kuinoa Everton

MKONGWE wa Manchester United, Wayne Rooney anatajwa kuwa huenda akarithi mikoba ya Rafael Benitez
ndani ya Goodison Park.


Everton siku ya Jumapili
ilimfuta kazi aliyekuwa kocha wake Rafael Benetiz baada ya timu hiyo kuendelea kufanya vibaya ndani ya Premier League.

 

Ushindi wa Norwich City wa mabao 2-1 dhidi ya Everton ndiyo ulipelekea kibarua cha kocha huyo kuota nyasi,
baada ya kocha huyo kudumu
hapo kwa miezi sita tu.


Inaelezwa kuwa kocha
huyo hakupewa fedha za kutosha kwaajili ya kufanya usajili kwani katika mechi 12 zao za
mwisho alipoteza tisa.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuondolewa Benitez, Rooney ndiye ambaye kwa sasa anainoa Derby County ya Championship ndiye anatajwa kuwa na nafasi
kubwa ya kutua kwenye
kikosi hicho.


Rooney ambaye
aliwahi kuichezea Everton anapewa nafasi ya kwenda kukinoa kikosi hicho zaidi japo kuna makocha wengine pia wanatajwa. Makocha kama Duncan Ferguson (msaidiz sasa) ambaye aliwahi kuishikilia kwa muda huko naye anatajwa kupewa timu

Leave a Comment