×

TFF Yawarudisha Waamuzi Wote Darasani

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), jana Jumatano liliweka wazi kuwa limeandaa semina ya siku tatu kwa
waamuzi wote wa Ligi
Kuu Bara kwa ajili ya kuwaandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.


Lengo kuu la semina
hiyo ni kutazama, kupitia changamoto na kuboresha maeneo mbalimbali ili kuondoa zile sintofahamu za uamuzi Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wadau mbalimbali wa soka juu ya changamoto za waamuzi kushindwa kuzitafsiri vema sheria za soka katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara zilizopita.

 

Katika malalamiko hayo, vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga walienda mbali zaidi na kuandaa
mkutano wa waandishi wa
habari juzi Jumanne kuelezea masikitiko yao na mwenendo wa baadhi ya waamuzi.

Stori na JOEL THOMAS, DAR

 

Leave a Comment