×

Vivo Wazindua Rasmi Simu Mpya Vivo 23 5G

 

HATIMAYE Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vivo Smartphones ya Tanzania, imefanikiwa  kuzindua rasmi simu mpya aina ya V23 5G Uzinduzi wa simu hiyo ya V23 5G, umefanyika Februari 28 mwaka huu, katika Ofisi zao kuu zilizopo ndani ya jengo la China Plaza Kariakoo jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa simu hiyo, Meneja Mauzo  wa Vivo nchini Tanzania, James Hujiang, amesema kuwa ukifanikiwa kununua na kumiliki  simu hiyo, basi jua  ina uwezo mkubwa wa kupiga picha kwenye mazingira yenye mwanga hafifu na kasi kubwa ya mtandao wa 5G.

 

“Cha kwanza kabisa ndani ya simu hii, ni kwamba V23 5G, ina kamera mbili za mbele zenye uwezo wa kupiga picha kwa upana na ukubwa zenye ubora zaidi, hata kama ni usiku, pia inakuwezesha kupata picha katika engo ya nyuzi 120 ambayo ni kama jicho la binadamu ambapo inakupa uwezo wa kuona engo zote bila kusuasua.

Mbali na hivyo simu hii ndiyo simu pekee ambayo inaweza kukufanya  kuwa na simu ya kwanza yenye  uwezo mkubwa kiasi cha kusukuma haraka internet kwa kasi ya 5G jambo ambalo ni adimu sana kwa sasa kupata simu yenye ubora mkubwa kama hii hapa nchini Tanzania, maana ina ram 8.

Kingine cha muhimu zaidi hii simu haiwezi kuibiwa na kuflashika kama ilivyo kwa simu nyingine kwani imewekewa Vivo Cloud yake ambapo yeyote akiiba hana uwezo wa kuitumia popote pale, ila pia ina uwezo mkubwa wa kukuruhusu kufungua App nyingi bila kukwama kwamba maana ina chip kubwa masafa zaidi ya 920,” alisema James Hujiang.

Leave a Comment