×

Urusi Yaongeza Majeshi Ukraine


Mazungumzo ya jana kati ya Urusi na Ukraine; mataifa ambayo yako vitani ni kama yamechochea moto wa mapigano.

 

Duru kutoka vyombo vya nchi za Magharibi vimetuhumu ongezeko kubwa la mashambulizi, kutoka majeshi ya Urusi, mengi kati ya hayo yakidaiwa kulenga kwenye makazi ya watu na kuua raia wakiwemo watoto.

 

Urusi imedaiwa kuongeza wanajeshi katika uwanja wa mapambano kutoka asilimia 40 ya mwanzo hadi kufikia 75.

Askari zaidi ya 70 wa Ukraine wanahofiwa kupoteza maisha ambapo rais wa nchi hiyo, Volodymyr Zelensky ameagiza wafungwa wenye ujuzi wa kupiga kuachiwa huru ili kushiriki katika vita.

 

Wakati huohuo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura azimio litakaloratibiwa na wajumbe wa Umoja wa Ulaya wanaoshirikiana na Ukraine kuishinikiza Urusi kusitisha mapigano.

ITAKULIZA! UJUMBE WA MWANAJESHI WA URUSI KWA MAMA YAKE KABLA YA KUUAWA, BALOZI WA UKRAINE AUSOMA…

Leave a Comment