
KAMPUNI ya Vivo leo Machi 14 katika studio za +255 Global Radio Imezindua rasmi aina mpya ya simu Vivo V23e, wakizindua simu hiyo maofisa kutoka Vivo wamesema simu hii inauzwa kwa gharama nafuu zaidi ili kila mtanzania apate fursa ya kuwa na simu hiyo.
Aidha Toleo hili halijaja hivi hivi Bali limekuja na zawadi kemkem kwa wateja wote watakao nunua simu hiyo pia uzuri wa simu za vivo huwezi kuziflash zikiibiwa au kupotea. Simu hii ipo madukani kwa Tsh 720,000 ikiwa na warranty ya miaka miwili.
Simu hii ina uwezo mkubwa wa kupiga picha hata kwenye mwanga hafifu ikiwa na camera yenye 64 MP ambayo inatoa picha angavu sana.
V23e imekuja na rangi mbili za kupendeza ambazo ni moonlight shadow na Sunshine Cost.