
Kampuni ya kielektroniki ya Samsung, imefanya mkutano katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki, wasambazaji na wafanyabiashara wa Tanzania wote, ambapo mkutano huo umeandaliwa na mkurugenzi mkuu mpya wa kampuni hiyo, Tae Sun Lee.
Lengo kubwa la mkutano huo ni kuwakutanisha wasambazaji na wafanyabiashara mbalimbali, kwa ajili ya kuboresha matumizi kwa watumiaji wa bidhaa za Samsung na kuonyesha bidhaa zao kama simu ambazo ni toleo la mwaka 2022.

Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa wanahakikisha bidhaa zao zinazidi kuwa bora siku hadi siku ili kuwezesha watumiaji wa bidhaa hizo duniani kote kupata furaha na faraja.
