
Mamlaka za Urusi zimeishutumu Ukraine kwa kufanya shambulio la anga kwenye ghala la mafuta katika eneo la Urusi.
Iwapo itathibitishwa – na Ukraine bado haijadai kuhusika na shambulizi la Belgorod, karibu na mpaka wa Ukraine – itakuwa mara ya kwanza kujulikana kwa ndege za Ukraine kupaa katika anga ya Urusi kulenga shabaha, na hivyo kuleta vita nchini Urusi.
Marubani wa helikopta za Ukraine wana uzoefu wa kutosha wa kuruka chini na kwa kasi ili kuepuka kutambuliwa na mifumo ya ulinzi wa anga na rada za kijeshi. Wamekuwa wakifanya hivyo haswa katika mkoa wa Donbas mashariki mwa Ukraine kwa miaka. Nilipata kushuhudia ujuzi wa ajabu wa marubani wa kijeshi wa Kiukreni mwaka wa 2018 – kuruka mita chache juu ya mstari wa miti ya telegraph.
Lakini ikiwa ripoti hizi ni sahihi – kuruka usiku, hadi katika eneo la Urusi, kuzindua shambulio kwenye ghala la mafuta la adui kungehitaji ushujaa wa ajabu – pamoja na ujuzi mzuri wa kuruka.
Helikopta zinazoruka chini bado ziko hatarini kwa mifumo ya ulinzi wa anga ya masafa mafupi. Kuruka usiku kungepunguza hatari hiyo, lakini kungeweza kuongeza hatari ya kugonga kitu karibu na ardhi.
Shambulio hili linalodaiwa pekee halitabadilisha vita kwa kiasi kikubwa. Lakini inaweza kuonyesha Ukraine imeweza kuweka jeshi lake la anga likifanya kazi, na kutoa msukumo mkubwa kwa ari ya jeshi la Ukraine.