
Kiungo wa Manchester United, Bruno Fernandes ameongeza mkataba mpya kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2026 mkataba huu ukiwa na kipingele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Baada ya kusaini mkata huo Bruno Fernandes ameweka wazi shahuku yake yakutaka kupata mafanikio zaidi akiwa na kikosi hicho kutoka jiji la Manchester.
“Kuna mengi zaidi nataka kufanya nikiwa hapa na ni vivyo hivyo kwa wachezaji wote na wafanyikazi wengine. Zaidi ya yote, tunataka kuwapa mashabiki mafanikio wanayostahili, tumekuwa pamoja katika nyakati nyingi za furaha, lakini mambo mazuri zaidi yanakuja kutoka kwangu na kwa timu kwa ujumla.” Amesema Bruno
Bruno raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Manchester United Januari mwaka 2020 katika dirisha dogo la usajili akitokea katika klabu ya sporting CP ya Ureno. Na tangu kajiunga na klabu hiyo tayari ameshaifungia timu hiyo mabao 49 katika michezo 117 katika michuano yote.