
Waweza tembelea sehemu tofauti lakini usiwe na maanani juu uzuri wa kipekee unaoipamba sehemu hiyo, ni sawa kutumia kidole kuchimba ardhini na usihisi mtetemo wake. Waswahili wana msemo usemao “tembea uyaone”, msisitizo si kutembea tuu bali ukiwa na yakini na hamu ya kutaka kuyafahamu yaliyoumbwa na Mwenyezi Mungu na maajabu yake katika uso wa dunia. haya ni makala ya video kuhus kisiwa Mbudya, kilicho ukanda wa pwani ya bahari ya hindi jijini Dar es salaam. Ni ndani ya Global TV pekee.