×

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan Aondolewa Madarakani, Alikuwa Anaipinga Marekani

Waziri Mkuu wa Pakistan aliyeondolewa madarakani Imran Khan.

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameondolewa mamlakani baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Washirika wake kadhaa na chama kikuu kwenye muungano na chama chake hawakumuunga mkono kwenye kura hiyo huku wakimlaumu kwa kusabisha kuanguka kwa uchumi wa Pakistan na kushindwa kutekeleza ahadi alizozitoa kwenye kampeni.

Khan awali alijaribu kuzuia kura hiyo kwa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema lakini Mahakama ya juu nchini Pakistan iliamuru kura hiyo iendelee. Upinzani ulishinda baada ya wabunge wapatao 174 kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Imran Khan. Bunge la Pakistan lina jumla ya viti 342

 

Spika wa bunge, Ayaz Sadiq alitangaza matokeo mapema leo Jumapili baada ya kumalizika zoezi hilo la kupiga kura lililochukua takriban saa 13.

Katikati: Shehbaz Sharif kiongozi wa upinzani anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Waziri Mkuu wa Pakistan.

Wabunge wachache tu wa vyama vilivyo katika muungano na chama cha Imran Khan cha Tehreek-i-Insaf au Vuguvugu la Pakistan la Haki waliohudhuria kikao hicho, yeye mwenyewe hakuhudhuria.

 

Waziri Mkuu Imran Khan mwenye umri wa miaka 67 ameondolewa baada ya kuiongoza Pakistan kwa miaka mitatu na nusu. Taifa hilo linalomiliki silaha za nyuklia lina idadi ya raia milioni 220. Jeshi limetawala nchini humo kwa karibu miaka 75, nusu ya historia ya nchi hiyo.

Wanajeshi nje ya Bunge la Pakistan.

Bunge linatarajiwa kukutana Jumatatu kumchagua waziri mkuu mpya. Shehbaz Sharif anayepigiwa upatu wa kupokea kijiti hicho cha uwaziri mkuu amesema hatua hiyo inafungua fursa ya mwanzo mpya.

 

Anasifiwa kuwa ni msimamizi mzuri. Sharif, mwenye umri wa miaka 70, ni mdogo wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif aliyeshikilia wadhfa huo mara tatu.

 

Zoezi la kupiga kura lilicheleweshwa kkutokana na kuahirishwa kwa mara kadhaa na hotuba ndefu za wabunge wa chama wa chama cha Khan, ambao waliilaumu Marekani kwa kuunga mkono njama ya kumwondoa Imran Khan nyota wa mchezo wa kriketi aliyegeuka mwanasiasa.

Wananchi wakiandamana kupinga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan.

Awali Khan aliilaumu Marekani kwa kuunga mkono hatua hizo za kumwondoa madarakani kwa sababu alikuwa ameitembelea Urusi na kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin mara tu baada ya Urusi kuivamia Ukraine mnamo Februari 24. Marekani imekanusha madai hayo.

 

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan aliyeondolewa madarakani alikuwa anaipinga Marekani katika kipindi chake chote, na atakumbukwa kwa kuunga mkono hatua yaTaliban ya kuirejesha Afghanistan mikononi mwake mwaka jana ambapo aliitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Taliban.

 

Muhammad Ali Khan, mbunge kutoka kwenye chama cha Imran Khan cha Tehreek-i-Insaf, amesema Waziri Mkuu huyo alipambana hadi mwisho na bila shaka atarejea uongozini hapo baadaye.

 

Khan akikuwa amesema hataitambua serikali ya upinzani, akidai bila ya kuwa na Ushahidi  kwamba kulikuwa na njama inayoongozwa na Marekani kumuondoa madarakani kwa sababu ya kusimama na Washington kuhusiana na masuala dhidi ya Urusi na China.

Amerudia kusema mara kadhaa kuwa vyama vya upinzani vya Pakistan vinafanya kazi na mataifa ya kigeni

Marekani imesema madai hayo “hayana msingi wowote”, na kwamba Bw. Khan hajawahi kutoa Ushahidi wowote.
Maafisa wa polisi mjini Islamabad, Pakistan, waliwakamata wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan wakati wa maandamano.

 

Alizuru Moscow kukutana na Rais Vladimir Putin wakati Urusi ikianzisha uvamizi wa Ukraine na hapo awali amekosoa kile ambacho utawala wa Bush ulikiita vita dhidi ya ugaidi.

 

Dakika chache kabla ya kura kuanza, spika wa bunge la Pakistani mshirika wa Bw Khan alitangaza kujiuzulu. Wanachama wa chama cha Bw Khan (PTI) waliondoka kwenye jumba hilo, wakisisitiza kuwa alikuwa mwathirika wa njama ya kimataifa.

DRONE VIDEO: DARAJA LILILOJENGWA na JWTZ na WANANCHI Pwani LAZUA UTATA, RAIA WATILIA SHAKA MIL. 167

Leave a Comment