
NYOTA wa Muziki nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz usiku wa kuamkia leo ameingia kwenye mkataba wa kuwa Balozi wa Mtandao wa Mawasiliano wa Airtel ambapo atakuwa na kazi ya kutangaza ubora na uimara wa huduma ya Airtel hasa matumizi ya Intaneti ya mtandao huo.
Kwa takribani siku kadhaa nyota huyo aliwaweka roho juu mashabiki wake baada ya kuwaambia kuwa atakuwa tayari kumtambulisha mpenzi wake mpya, huku akizua shauku kubwa kwa mashabiki hao kwenye moitandao ya kijamii kwa kutaka kujua ni mpenzi gani atakayetambulishwa na Diamond Platinumz “Simba”
Sasa ni rasmi Diamond Platinumz ni Balozi mpya wa Mtandao wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania.