
Habari inayotrend kwa kasi kubwa kwenye mitandao ya kijamii kwa leo, ni madai kuhusu mastaa wawili wakubwa wa muziki nchini Marekani, Rihanna na A$AP Rocky kudaiwa kumwagana, chanzo kikiwa ni usaliti ambao Rocky ameufanya kwa Rihanna a.k.a mama kijacho.
Aliyeibua tetesi hizo ni blogger maarufu wa fasheni, Louis Pisano ambapo kupitia akaunti yake ya mtandao wa twitter, aliandika kwamba wawili hao wameachana baada ya A$AP Rocky kumsaliti Rihanna kwa kutoka na mwanamitindo wa viatu, Amina Muaddi wakati Rihanna akiwa mjamzito.
Muda mfupi baadaye, ‘twiti’ hiyo ilikuwa imesambaa kwa kasi kubwa mitandaoni, huku mashabiki wengi wa Rihanna wakiwa ni kama hawaamini kama A$AP Rocky anaweza kumpiga tukio Rihanna, tena akiwa na ujauzito mkubwa akiwa karibu kujifungua.
Taarifa zinaeleza kwamba Amina ni mfanyakazi wa Rihanna katika lebo yake ya viatu ya Fenty Footwear na amekuwa akimdizainia viatu mbalimbali anavyovivaa mwanadada huyo na ukaribu wao ndiyo uliomfanya A$AP Rocky atoke naye kimapenzi.

Si Rihanna wala A$AP Rocky aliyejitokeza kutolea ufafanuzi suala hilo au kuthibitisha kama ni kweli au laa, pengine muda utazungumza.