×

Mbunge wa Buchosa Ashiriki Mazishi ya Maunda Zorro, Awapa Pole Familia – VIDEO

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo akimpa pole kaka wa marehemu Maunda Zorro, Banana Zorro eneo la makaburini Toangoma Kigamboni Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo akimpa pole Baba Mzazi wa marehemu Maunda Zorro wakati wa kuusindikiza mwili wa mpendwa wao eneo la makaburi yaToangoma Kigamboni Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Muvies wakiwa eneo la makaburini kuusindikiza mwili wa marehemu Maunda Zorro eneo la Toangoma Kigamboni Dar es Salaam.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika kuusindikiza mwili wa aliyekuwa msanii hapa nchini Maunda Zorro aliyefariki dunia juzi katika ajali ya gari huko toangoma Kigamboni Dar es Salaam.
Miongoni mwa watu mashuri waliohudhuria wakati mwili huo ukizikwa ni Mbubge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Group ambapo akiwa amejumuika na waombolezaji wengine amewapa pole wafiwa akiwemo baba mzazi wa Maunda Zoro na kaka wa marehemu ambaye pia ni msanii Banana zoro.
Mwili huo umezikwa katika makaburi yaliyoko jirani na nyumbani kwake alikokuwa akiishi marehemu maunda zorro eneo la Toangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

ITAKUGUSA! MBUNGE SHIGONGO AFIKA MSIBANI, TAZAMA ALIVYOMFARIJI BANANA, HARMONIZE AKISHUHUDIA

Leave a Comment