×

OPPO Yaja na Reno 7 4G na 5G Hizo ni Kiboko

Meneja Mafunzo wa OPPO Farida Mwangosi kushoto na Msimamizi wa mauzo, Venance Chiwalala wakiwa katika uzinduzi wa simu hizo.

 

 

Kampuni ya simu ya OPPO imezindua simu yake mpya hapa nchini ya Reno 7 4G na 5G.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Meneja Mafunzo wa OPPO hapa nchini, Farida Mwangosi amesema kampuni hiyo inayowajali wateja wake imeamua kuja na simu hiyo ili kuboresha maisha ya wateja wao.

Akiizungumzia OPP Reno 7 4G meneja Farida amesema ubora wa simu hiyo unaanzia kwenye muonekanao ambapo wa kasha la ngozi na kuifanya iwe na mvuto wa aina yake.

Akielezea upande wa kamera amesema kamera zake zimetengenezwa kwa ukubwa zaidi kwa ajili ya kutoa picha zenye ubora wa hali ya juu kama zilivyo.

Amesema simu hiyo ina Ram 8 na GB 256 na unaweza kuongeza Ram kufikia mpaka 13 na ina prosesa kubwa inayofanya simu hiyo kuwa na kasi ya aina yake.

Akizungumzia kioo amesema ina kioo kipana kinachomfanya mtumiaji aweze kufurahia muvi na picha wakati akiipruzi simu hiyo.

Upende wa betri amesema simu hiyo inabetri inayodumu kwa muda mrefu na unapoichaji hujaa ndani ya muda mfupi.

Baada ya uzinduzi huo meneja Farida amewataka wateja wote wanaohitaji simu hiyo kufika maduka yanayouza simu za OPPO na kuagiza simu hizo ambapo utaweza hata kuweka pesa kidogokidogo kuanza shilingi elfu 70,000 na utapatiwa zawadi ya spika ya blue tooth ambayo ni maalum kwa ajili ya wateja wa simu za OPPO alimaliza kusema meneja Farida.

Naye Msimammizi wa mauzo wa kampuni hiyo Venance Chiwalala kwa upande wake aliitambulisha OPPO Reno 7 5G na kuelezea sifa kemkem zilizomo kwenye simu hiyo.

Chiwalala alianza na kuelezea sifa kubwa ya simu hiyo ambayo ni wireless PC ambapo unaweza kuinganisha na computer bila waya na kuhamisha data na kufanya mambo mengine yanayohitaji kutumia nyaya kwa simu zingine.

Akielezea upande wa kamera amesema kamera zake zinaubora wa hali ya juu na kuweza kumafa mtumiaji aweza kupiga picha katika mazingira tofauti na kujichagulia rangi za picha anayoitaka kupiga.

Pia Chiwalala amesema simu hiyo imepewa daraja A na kampuni ya TV ya TUVSDU.

Kwa kumalizia amesema simu hiyo inapatikana madukani kwa bei elekezi ya shilingi 1,250,000.

Leave a Comment