
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amefanya ziara ya ghafla mjini Kyiv na kukutana na Rais wa Ukraine
Katika ujumbe wa tweet iliyo na video fupi inamuonesha Pelosi katika mitaa ya mji mkuu wa Ukraine, Rais Zelensky alisema “Marekani ndio inayoongoza kwa kuunga mkono vita vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi”.
“Asante kwa kusaidia kulinda mamlaka na uadilifu wa eneo la jimbo letu!”
Pelosi aliandamana na Mwanademokrasia mwenzake Adam Schiff na wabunge wengine watatu.
Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri wa ulinzi Lloyd Austin mwishoni mwa juma lililopita ilithibitishwa rasmi na Ikulu ya White House baada ya kuondoka nchini humo.