×

Watu 5 Wapoteza Maisha kwa Kufukiwa na Kifusi cha Udongo Songwe.

Zoezi la Uokoaji likiwa linaendelea eneo la tukio

WATU 5 katika familia mbili tofauti wamepoteza maisha kwa kufukiwa na kifusi cha udongo kilichoporomoka kutokana na mvua zilizonyesha usiku wa tar 29/04/2022 Wilaya Ileje Mkoani Songwe.

Wakazi wa Wilaya ya Songwe

Mashuhuda wa tukio hilo katika kata za Sange na Ngulugulu wilayani humo wanasema mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia April 29 na kusababisha kuporomoka kwa udongo uliosababisha kubomoka kwa nyumba mbili moja katika kata Sange iliyokuwa na wanafamilia watatu baba mama na mtoto mmoja, pia katika kata ya Ngulugulu ambapo familia ya mke na mume walipoteza maisha.

 

Mkuu wa mkoa wa Songwe Mh Omary Mgumba ametoa pole kwa wafiwa pamoja na wananchi wote wilayani humo.

Leave a Comment