×

Ajali ya Gari na Treni Mkoani Morogoro Yasababisha Kifo cha Mtu Mmoja

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Fortunatus Musilimu amethibitisha kuwa mtu mmoja ambaye ni mmiliki wa gari aina ya Toyota Pick Up yenye namba za usajili T 840 DQF amefariki katika ajali ambayo gari lake liligonga Kiberenge cha Treni na kusababisha ajali mbaya iliyochukua uhai wake, mbali na kifo hicho kuna majeruhi mmoja ambaye tayari ameshapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu

 

Kamanda Muslimu amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya sa sita na nusu usiku na majeruhi aliyeokolewa anafahamika kwa jina la Ladhia Kassim.

Leave a Comment