×

Trump: Acheni Kutoa Misaada Ukraine, Angalieni Usalama wa Wanafunzi Wetu Kwanza

Donald Trump akiongea kwenye mkutano wa udhibiti wa matumizi na biashara ya bunduki nchini Marekani (Pro-gun Conference)

RAIS wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema Marekani lazima iachane na matumizi ya pesa yasiyokuwa ya lazima ya kuisaidia nchi ya Ukraine ambayo ipo kwenye vita dhidi ya Urusi na badala yake iwekeze kwenye kuhakikisha inatengeneza mazingira mazuri na usalama wa watoto wao ambao wanauawa bila hatia kwa kupigwa risasi mashuleni.

 

Trump ameyasema hayo kufuatia tukio la hivi karibuni la watoto 19 na walimu 2 kuuawa kikatili kwa kupigwa risasi na kijana aliyekuwa na bunduki na kuvamia eneo la shule Jimbo la Texas, Marekani.

 

“Tunatakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha usalama wa watoto kwenye miji yetu.” Trump aliongea hayo wakati wa mkutano kuhusu kupunguza matumizi na biashara za Bunduki nchini Marekani maarufu kama (Pro-gun Conference).

Baadhi ya waandamanaji wakipinga matumizi na sera za umiliki wa silaha nchini Marekani

Trump aliendelea kwa kusema:

 

“Tulitumia Trilions nchini Iraq na Afghanistan na hatukuambulia chochote,kabla hatujajenga nchi za wenzetu na dunia kwa ujumla, ni lazima tujenge shule nzuri na salama kwa watoto wetu ndani ya taifa letu.” Aliongea Trump huku akishangiliwa na umati wa wasikilizaji.

 

Katika hotuba yake Trump amegusia umuhimu wa kila raia wa Marekani ambaye hana rekodi mbaya ya matukio awe na silaha kwa ajili ya kujilinda yeye na familia yake, amedai njia pekee ya kupambana na mtu mbaya mwenye bunduki ni mtu mzuri kuwa na bunduki.

 

Mapema mwezi huu Baraza la Congles la Marekani lilipiga kura kupeleka zaidi ya dola Bilioni 40 kama msaada wa kivita Nchini Ukraine. Kwa ujumla Marekani imetumia zaidi ya dola Bilioni 54 kama pesa ya msaada kwa Ukraine tangu nchi hiyo ivamiwe na Urusi mwezi Februari mwaka huu.

 

 

Leave a Comment