×

Rasmi Kajala Awa C.E.O na Meneja wa Harmonize, Choppa Afunguka

Kajala Frida

 

BAADA ya Harmonize kuthibitisha kurudiana na Kajala, taarifa mpya kutoka Konde Gang ni kwamba, rasmi Kajala atakuwa C.E.O na meneja wa Harmonize kwenye kazi zake na biashara zote ambazo anafanya.

 

Taarifa hiyo ilitolewa na Rajab Mchopa ambaye ni kiongozi wa juu kwenye ‘menejimenti’ ya Harmonize na Konde Gang, Choppa aliweka habari hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Harmonize

Choppa aliandika: “Allow me to welcome in management team new C.E.O and manager Kajala Frida i’m excited to work with you shem.”

 

Naye Harmonize alishusha komenti kwenye posti hiyo akisema: “Big Team, Big Dream.” Chini yake Kajala akiachia emoj za moto na kuonyoosha mikono juu.

 

Itakumbukwa Harmonize, kabla hajarudiana na mpenzi wake Kajala, aliwahi kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba anatamani siku moja akirudiana na Kajala, basi mrembo huyo awe meneja wake.

 

Hivyo Konde kwa sasa anasimamiwa na watu wanne, Beauty Mnali ‘Mjerumani’, Kajala, Jembe ni Jembe na Choppa.

GSM YAUNASA MKATABA WA STRAIKA MZAMBIA, SAIDOO ASIMULIA MAZITO | KROSI DONGO

Leave a Comment