×

Hatua ya Mwisho kwa Ndejembi Bungeni, Waziri Ammwagia Sifa (Picha +Video)

Makamu wa Rais Mteule na Waziri wa Nishati, Deogratius John Ndejembi, leo Agosti 28, 2026, amehudhuria Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Tatu kinachoendelea jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewasilisha hoja ya kumthibitisha Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua hiyo imekuja baada ya Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, kutangaza kuwa amepokea jina la Makamu wa Rais Mteule lililowasilishwa kwake na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

Ndejembi, ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino na Waziri wa Nishati, alipendekezwa na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kujiuzulu nafasi hiyo.

Endapo Bunge litamthibitisha, Ndejembi ataingia rasmi katika nafasi ya Makamu wa Rais na kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leave a Comment