
JUKWAA mahususi kwaajili ya wagonjwa yaani ‘Universal Patient Portal’ linalojiendesha kikamilifu kiteknolojia kuendana na mnyororo (Blockchain technology) ambalo litabadilisha sura ya utoaji huduma za kiafya kwa wagonjwa kote Afrika na ulimwenguni limezinduliwa.
Kupitia jukwaa kuu salama (Myrekod.com) wagonjwa na wataalamu wa afya watapata taarifa kwa wakati halisi na historia ya matibabu ya mgonjwa. Pia wataweza kuhakikisha usimamizi mzuri unaoendelea wa matibabu na kupata habari muhimu, kwa wakati unaofaa katika dharura.
Mkurugenzi Mtendaji wa AfyaRekod, John Kamara, alisema AfyaRekod ilianzishwa mwaka 2019 chini ya uangalizi wa Adanian Labs na ufadhili kutoka kwa Mac Venture Capital na Next Chymia.
Kamara aliweza kujionea mwenyewe jinsi ukosefu wa taarifa sahihi za matibabu zinavyoweza kusababisha maamuzi yasiyo sahihi kimatibabu pindi alipompoteza rafiki wa karibu kwa kukosa taarifa zilizo sahihi wakati wakuugua kwake.
Kamara aliunda jukwaa hili la intelijensia bandia (AI) ambalo lingefuatilia taarifa za mgonjwa, linalolenga kuziba pengo kati ya huduma ya afya na matibabu, mahali popote, wakati wowote kwa wagonjwa, wataalamu wa matibabu, watoa huduma za afya na mashirika.
Taarifa za matibabu ni nyenzo muhimu katika kudhibiti afya, kuwaarifu wataalam wa huduma ya afya kuhusu dawa, magonjwa sugu, matatizo na matibabu ya zamani na hatimaye kutambua na kubainisha njia sahihi zaidi ya matibabu.
Utambuzi mbaya unaweza kusababisha kuchelewa kwa matibabu sahihi. Taarifa ya IOM iliyotolewa mwaka 2015 ilionyesha kuwa karibu visa milioni 12 vya utambuzi mbaya wa wagonjwa hutokea kila mwaka nchini Marekani, nchi yenye sekta ya afya iliyostawi vizuri.
Utambuzi mbaya unaweza kuzuilika, lakini tu ikiwa taarifa za afya ni sahihi, na kufikika kirahisi. “Moja ya tatizo kubwa linapokuja suala la upatikanaji wa afya bora baŕani Afŕika ni taarifa (data). Ukusanyaji wa taarifa ni mdogo na taarifa zinazopatikana hazijitoshelezi katika hospitali au vituo vya afya na hilo ndilo tunalojaribu kulibadilisha kupitia AfyaRekod.
Tunafanya ukusanyaji wa taarifa za wagonjwa, Pamoja na uhamishaji wa taarifa uwe rahisi na utambulisho wa kidijitali unaojitegemea, na kwa njia hiyo tunaweza kuunda huduma bora ya afya.
Kupitia jukwaa la AfyaRekod, wagonjwa wataweza kutengeneza mfumo wenye taarifa zao zote za afya, za zamani na za sasa na kupata rekodi zao wakati wowote”, aliongeza Irene Kiwia, Mwanzilishi Mwenza wa AfyaRekod.
Janga la UVIKO 19 limeharakisha na kuzidisha umuhimu katika kuongeza nguvu kasi ya upatikanaji wa taarifa za afya na uchanganuzi.
Hili ni tatizo la kimataifa ambalo limeshughulikiwa kwa mafanikio kupitia jukwaa la AfyaRekod ambalo linatumia ubunifu wa kiteknolojia kumpa mgonjwa kipaumbele.
Zaidi, wagonjwa wanaweza kusimamia taarifa za afya zao, ikiwa ni pamoja na maagizo na muhtasari wa ziara ya hospitali.
AfyaRekod Universal Patient Portal inatoa suluhisho salama la kuhifadhi na kupata taarifa zako za afya kwa njia ya simu au kompyuta na kwa weledi.
Suluhisho hizi ni pamoja na; rasilimali za afya, ufuatiliaji wa dalili, vikumbusho na viarifa, pamoja na uhamishaji wa taarifa kwenye chaneli na nyenzo nyingi.
Ingawa mgonjwa yeyote anaweza kutumia zana hizi, mtandao huu ni muhimu zaidi kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu, wazazi, wajawazito na wagonjwa wenye magonjwa ya kurithi.
Jukwaa la AfyaRekod linajumuisha pia madaktari, wanaotoa kliniki ya kidijitali yenye jukwaa la B2B, mifumo ya duka la dawa kwa njia ya simu na maagizo ya matibabu kwa mtandao.
Kwa watoa huduma, jukwaa lina vipengele vingi vya utendaji kama vile usimamizi wa hospitali, usimamizi wa wagonjwa, usimamizi wa maarifa na usimamizi wa orodha, pamoja na zana ya kutoa taarifa inayoendeshwa na akili bandia (AI), ambayo huruhusu mashirika kufanya maamuzi ya kimkakati, utabiri na utambuzi wa mapema kwa kutumia uchanganuzi wa taarifa.
Mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika mengine yanayohusiana yanaweza kusajili na kudhibiti makundi yanayolengwa kwenye jukwaa.
AfyaRekod ni Sehemu ya mpango wa NVIDIA AI kupitia AICE Africa na ina watumiaji zaidi ya 150,000 nchini Kenya pekee na inazinduliwa mwezi julai nchini Nigeria, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia.
AfyaRekod inapatikana kupitia programu (android na iOS) na tovuti kupitia myrekod.com
Washirika muhimu wa AfyaRekod ni pamoja na The Association of Sisterhoods of Kenya (AOSK), Healthy Mind Foundation(Nigeria), Alchemy (Afrika Kusini), AURA (Afrika Kusini), GE Healthcare, Telkom, The Africa Block-Chain Center, The AI Center of Excellence, Adanian Labs, na Lishe Living miongoni mwa wengine.
Kwa sasa katika bidhaa zao za kibiashara B2B, AfyaRekod inatumika na hospitali zaidi ya 50.
Fuata AfyaRekod kupitia:
Facebook | Twitter | Instagram | LinkedIn
Tovuti: https://afyarekod.com/
Kwa kuwasiliana na AfyaRekod;
Zainab Abdallah,
Meneja Masoko na Mawasiliano – Adanian Labs
Simu no: 0743255628