×

Airtel Yahitimisha Promosheni ya Tesa Kimilionea, Yaahidi Neema Nyingine

Meneja Chapa wa Airtel Money, Gillian Rugumamu (kushoto) akihitimisha promosheni hiyo kwa kuchezesha droo ya mshindi wa Toyota Rav 4 ya mwisho. Kulia ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga akihakiki uchezeshwaji wa droo hiyo.

 

 

KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya Aitel Money, leo imefikia kilele cha promosheni yake ya Tesa Kimilionea.

Sehemu ya wanahabari nao wakishuhudia uchezeshwaji wa droo hiyo.

 

 

Katika Promosheni hiyo wateja na mawakala wa Airtel Money waliokuwa wakifanya miamala walikuwa wakijishindia zawadi mbalimbali kila siku ambapo zawadi kubwa kwa siku ilikuwa shilingi milioni moja na kila mwezi walikuwa wakipatikana washindi wawili mshindi wa milioni 10 na gari mpya aina ya Toyota Rav 4.

Mshindi wa shilingi milioni moja, Josephine Michael Mlyambongo akipokea shilingi milioni moja kutoka kwa Meneja Chapa wa Airtel Money, Gillian Rugumamu. Anayeshuhudia katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.

 

 

Akizungumza makao makuu ya Airtel Jijini Dar leo, Meneja Chapa wa kampuni hiyo, Gillian Rugumamu amesema;

 

“Kwa miezi isiyopungua sita tulikuwa tukiendesha promosheni yetu ya Tesa Kimilionea ambapo kila siku wateja wa Airtel Money na Mawakala wake walikuwa wakijishindia shilingi milioni moja”.

Meneja Chapa wa Airtel Money, Gillian Rugumamu akimpa mkono mshindi wa milioni moja, Vasta Anjero Mtasiwa (kushoto) wakati akijiandaa kumpa mkwanja wake.

 

 

Gillian aliendelea kusema kuwa katika promosheni hiyo kila mwezi wateja wetu hao na mawakala walikuwa wakipata washindi wakubwa wawili ambapo mmoja alikuwa akipata shilingi milioni 10 na mwingine gari jipya aina ya Toyota Rav 4. Alisema Gillian.

 

“Naomba nichukue nafasi hii kuwaambia wateja wetu pamoja na mawakala wetu kuwa leo ndiyo tumefikia kilele cha promosheni yetu hii ya Tesa Kimilionea endeleeni kutumia huduma za airtel money mambo mengine mazuri zaidi yanakuja.

 

Katika kuhitimisha droo hiyo washindi wengine wawili walipatikana ambapo dereva mmoja mkazi wa Kiondoni Dar alijishindia shilingi milioni 10 na muuza nyanya wa soko la Tegeta Nyuki, Dar alijishindia Toyota Rav 4.

Leave a Comment