×

Muuza Madawa ya Kulevya Maarufu wa Mexico Rafael Quintero Akamatwa

Rafael Caro Quintero akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa nchini Mexico

Mamlaka nchini Mexico zimemkamata mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya Rafael Caro Quintero, ambaye alikuwa kwenye orodha ya FBI ya wahalifu 10 wanaotafutwa zaidi duniani, Quintero amekuwa akitafutwa na Marekani kwa tuhuma za mauaji aliyowahi kuyafanya nchini humo.

Quintero mwenye umri wa miaka 69, anakabiliwa na mashaka nchini Marekani baada kuamuru kutekwa nyara, kuteswa na kuuawa kwa wakala maalum wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DEA) Enrique “Kiki” Camarena mwaka 1985.

Hii ni Oparesheni nyingine ambayo imefanikiwa  baada ya mwaka 2014 Marekani kwa kushirikiana na Mexico kufanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara maarufu wa madawa ya kulevya  Guzmán Loera maarufu kama El Chapo.

Leave a Comment