×

Muuza Nyanya Akabidhiwa Gari, Mkulima Aondoka na Milioni Kumi za Airtel Money

Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda akimkabidhi mfano wa funguo mshindi wa gari mfanyabiashara wa nyanya wa Soko la Tegeta Nyuki Dar, John Mathayo. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa huduma za Airtel Money Maria Mwanyale na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.

 

KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi ya Airtel ambayo ilikuwa ikiendesha promosheni ya Tesa Kimilionea kupitia huduma ya Airtel Money, leo imehitimisha promosheni hiyo kwa kuwakabidhi washindi wa droo ya mwisho zawadi zao.

Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda (kushoto) akimpongeza Mnyamulu Dyamwale wakati akimkabidhi mfano wa hudi ya milioni kumi alizojishindia. Wanaoshuhudia kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na wa pili kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za Airtel Money Maria Mwanyale.

 

 

Washindi hao walikabidhiwa zawadi zao kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel, Kinondoni Morocco jijini Dar, ambapo mfanyabiashara ya nyanya wa Soko la Tegeta Nyuki Dar, John Mathayo alijishindia gari jipya aina ya Toyota Rav 4 na mkulima Mnyamulu Dyamwale aliondoka na kitita cha shilingi milioni kumi.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akizungumza kwenye hafla hiyo, kulia ni mshindi wa gari, John Mathayo na kushoto ni mshindi wa milioni kumi Mnyamulu Dyamwale.

 

 

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi zawadi hizo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda alisema kampuni inayofuraha kubwa sana kuwakabidhi washindi hao zawadi hizo walizojishindia kwa kutumia huduma za Airtel Money kwa kufanya miamala na kufanya malipo mbalimbali ikiwemo Luku, faini za Polisi  na mengineyo.

 

“Leo tukiwa tunahitimisha promosheni ya Tesa Kimilionea kwetu Airtel ni siku ya furaha kubwa sana kuwakabidhi wateja wetu hawa zawadi zao ambapo mshindi wa kwanza tunamkabidhi gari jipya aina ya Toyota Rav 4 na mshindi wa pili pesa taslimu shilingi milioni kumi.

 

“Kwa kuhitimisha promosheni hii tunawaomba wateja wetu waendelee kutumia huduma za Airtel Money kwa kupiga *150*60# na kufanya miamala na kulipia huduma mbalimbali kwani mwisho wa promotion hii ndiyo mwanzo wa promosheni nyingine kabambe inayokuja. Alisema Mkurugenzi Nchunda.

Leave a Comment