×

Fenerbahce Yapigwa Faini na UEFA kwa Kosa la Kushangilia Jina la Putin

Mashabiki wa Fenerbahce ya nchini Uturuki

KLABU ya Fenerbahce ya nchini Uturuki imeambulia nyundo ya kufungiwa sehemu ya uwanja wa klabu hiyo kutoingiza mashabiki kwa kipindi cha miaka miwili katika mashidano yanayosimamiwa na Uefa kutokana na kuimba jina la Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mchezo wao wa kufuzu kucheza mashindano ya UEFA.

 

Sambamba na adhabu hiyo klabu pia imepigwa faini ya Euro 50,000 na Kamati ya Maadili ya UEFA.

 

Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Ulaya UEFA imesema:

Fenerbahce wamepigwa pia faini ya Euro 50,000

“Adhabu imetokana na kurushwa kwa vitu pamoja na kutamka maneno yenye uchochezi na yanayokashfu watu.”

 

Kifungo hicho kimeathiri zaidi ya siti 5,000.

Leave a Comment