×

Kim Jong Un Atangaza Ushindi Dhidi ya COVID-19, Siri Nzito Yafichuka

Kim Jong Un

RAIS wa Korea kaskazini Kim Jong Un amesema nchi yake imefanikiwa kumaliza tatizo la Covid -19 na hakuna kisa hata kimoja kilichoripotiwa hadi sasa.

 

Kim Jong Un amesema “hakuna kisa hata kimoja cha homa kinachoshukiwa kuhusishwa na virusi hivyo kilichoripotiwa tangu Julai 29, 2022” na analaumu mlipuko wa awali wa vipeperushi vilivyopeperushwa mpakani kutoka Korea Kusini.

Kim Jong Un ameishutumu Korea Kusini kwa kusababisha maambukizi ya Covid-19 nchini mwake

Katika hali hiyo dada wa kiongozi huyo anayejulikana kama Kim Yo-Jong ametanabaisha kuwa kiongozi huyo amekiri alipata “homa” wakati wa mlipuko huo.

Kim Jong Un

Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini (KCNA) liliripoti siku ya Alhamisi kwamba dadake Kim, Kim Yo Jong, alisema kaka yake alikuwa na “homa” na akalaumu mlipuko wa Korea Kaskazini kwa vipeperushi vilivyopeperushwa kuvuka mpaka kutoka Korea Kusini.

 

Leave a Comment