×

Polisi Wanawawinda Washukiwa Baada ya Mauaji Huko Saskatchewan Nchini Canada

Polisi wanawawinda washukiwa baada ya mauaji

POLISI nchini Canada wameanzisha msako mkali kuwasaka watu wawili wanaoshukiwa kuwaua kwa kuwachoma visu takriban watu 10 katika shambulio ambalo limeshangaza taifa.

 

Washukiwa wawili waliotajwa kama Damien Sanderson na Myles Sanderson wapo mafichoni na wanachukuliwa kuwa na silaha.

 

Vituo vya ukaguzi vimewekwa katikati mwa mkoa wa Saskatchewan, huku wakazi wakihimizwa kujificha ndani ya nyumba na kuwa waangalifu sana wanapoendesha msako.

 

Waathiriwa wa tukio hilo walipatikana katika maeneo 13 katika jamii ya kiasili ya James Smith Cree Nation na Weldon. Ikiwa watu 10 walipoteza Maisha na wengine 15 walijeruhiwa katika tukio hilo.

Watu 10 wamefariki na wengine zaidi ya 15 kujeruhiwa

Ni moja wapo ya vitendo vikali zaidi vya unyanyasaji mkubwa ambavyo Canada haijapata kuona. Waziri Mkuu Justin Trudeau alitaja mashambulizi hayo kuwa “ya kutisha na ya kuvunja moyo”.

Ni tukio la kutisha na kuvunja moyo

Washukiwa hao walionekana mara ya mwisho na umma huko Regina wakati wa chakula cha mchana siku ya Jumapili, na huenda walikuwa wakisafiri kwa gari nyeusi aina ya Nissan Rogue.

Imeandikwa na:John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment