
Dar es Salaam, Alhamisi Septemba 15, 2022 BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambayo imeorodheshwa kwenye soko la hisa la London imepiga hatua nyingine kwenye soko baada ya kuzindua kampeni maalum inayolenga kuwanufaisha wateja wanaofungua akaunti za amana.

Kwenye kampeni hiyo ambayo inaanza leo na kuendelea mpaka Desemba 15 mwaka huu 2022, wateja wa BancABC Tanzania wanaofungua akaunti za amana watapata riba ya hadi ya asilimia 11 papo hapo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua kampeni hiyo, Afisa Mkuu Muendeshaji BancABC Tanzania, Joyce Malai alisema kuwa benki hiyo imezindua kampeni hiyo ambapo wateja wanaofungua akaunti za amana watapata riba ya asilimia 11 kuanzia leo mpaka katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.
Riba hiyo italipwa papo hapo huku salio la akaunti likiendelea kubaki salama mpaka muda wa ukomavu utakapofika. “Hii ni moja ya ofa bora zaidi kwenye soko na naomba kutumia fursa hii kuwaomba wateja wetu na Watanzania wengine ambao hawana akaunti kwenye benki yetu kutumia nafasi hii kufaidika na kampeni hii, unavuna kabla ya kupanda.” Alisema Malai.
Malai alisema kuwa BancABC imejidhatiti kufikia mahitaji ya wateja na kuhakikisha kwamba wanakuwa pamoja na benki hiyo. Tunathamini jinsi wateja wetu wanavyotuunga mkono na hiyo ndiyo sababu sisi kama benki tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe.”
Aliongeza kuwa BancABC ipo tayari kukubali wateja kufungua akaunti za amana kwa kipindi cha robo ya mwaka , nusu au mwaka na riba italipwa hapo hapo kwa akaunti zote hizo. “ Sisi kwetu mteja ni mfalme ndio sababu tuko tayari kumsikiliza” Malai alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Kitengo cha Wateja wa rejareja na Biashara, Lilian Mwakitalima alisema kuwa kinachotakiwa kufanywa na mteja yeyote ili aweze kujipatia ofa hii ni kufika kwenye matawi yetu yaliyopo nchini kote na kufungua akaunti za amana ya muda maalum ambapo riba hiyo italipwa papo hapo, lengo ni kukupa uhuru wa kupanga kwa sasa au baadae.
“Mteja anapaswa kutembelea tawi lolote la BancABC Tanzania na kufungua akaunti ya amana na riba yake kulipwa hapo hapo, mteja anaweza kutumia riba kufan ya manunuzi, kufanya matembezi au kuwanunulia zawadi wanafamilia au marafiki,” Mwakitalima aliongeza.
“Mteja pia anaweza kutumia akaunti hii ya amana kupata mkopo. Tunakaribisha wateja watutembelee kwani sisi tuko huru kuwasikiliza”, alisema Mwakitalima.
Alimalizia kwa kusema kuwa mteja anaweza kuwasiliana nao kwa kupiga 0779111000 au kutembelea moja kwa moja matawi yao yaliyopo Dar es Salaam, Dodoma,Mwanza na Arusha, kisha kufungua akaunti ya amana na kuanza kufaidika.