×

Safari ya Afrika Yamsaidia Lewis Hamilton Kujihisi Amani, Azigusia Tanzania, Kenya na Namibia

Lewis Hamilton

BINGWA wa mashindano ya magari ya formula 1 Lewis Hamilton ambaye ana rekodi ya kuchukua ubingwa wa Dunia mara saba afurahishwa na safari yake ya Afrika kwa kuwa amejihisi kupata amani kutokana na changamoto ambazo huwa anapitia katika kazi yake ya mashindano ya formula 1.

 

Lewis Hamilton amesema amesubiri mpaka kufikisha miaka 30 ndipo ametaka kutambua uhalisia wa jina lake la Hamilton, wao ni watu wa wapi na watumwa wote walioingia Caribbean walitokea wapi.

 

Dereva huyu ambaye ni kijana pekee mweusi aliyepata bahati ya kuwa dereva wa mashindano ya magari ya formula 1 amesema:

 

.”Nakumbuka presha niliyokuwa nayo ya kuwa tofauti na madereva wengine ilinibidi kuongea tofauti, kuwa tofauti kipindi nipo katika shirika hili ambapo nilikuwa nimezungukwa na watu weupe”

Hamilton akiwa nchini Tanzania

Wakati Hamilton akikumbukia shida alizopitia hapo zamani kama vile baba yake mzazi kutafuta na kufanya kazi mbili ili aweze kutimiza ndoto za kijana wake, Formula 1 haikuwa ni mchezo ambao mtu kama Lewis Hamilton alionekana kufaa kushiriki kwa sababu za ubaguzi wa rangi hivyo alipitia changamoto nyingi mpaka kujulikana kama dereva bingwa wa magari ya Formula 1.

 

Kwa mujibu wa Hamilton ni kwamba Bara la Afrika lina nishati za asili ambazo hupelekea mtu kujihisi amani, Hamilton hakuwa na hamu ya kutembelea mahali penye biashara kubwa na majengo ya kifahari japo anafahamu kuwa sehemu kama hizo zipo katika Bara la Afrika lakini yeye alipendelea zaidi kwenda sehemu ambazo watu walikuwa wanaishi kwa chochote wanachokipata.

 

Hamilton akiwepo Afrika aliweza kutembelea Tanzania, Kenya, Rwanda na Namibia akijihisi ni mtu mpya kabisa,

aliandika katika mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kusema:

Lewis Hamilton ameshinda mataji saba ya Formula One

” Nimetumia muda na watu wa Pokot huko nchini Kenya na kuwepo nao tu ilikuwa ni kitu, kukaribishwa ilikuwa ni kitu tofauti na cha heshima ambacho siwezi kukichukulia kirahisi. Jinsi nilivohisi hapa ni kama ambavyo nahisi nikiwa na familia yangu huko nyumbani. Sisi sote ni familia hata hivyo nitabeba uzoefu na kumbukumbu nilizopata kutoka Kenya katika safari hii kiujumla moyoni mwangu milele.”

 

Kwa sasa Hamilton anasema anajihisi furaha na pia hasumbuliwi na kuisha kwa ushindi wake wa mfululizo kama ilivokuwa hapo awali, anafurahishwa na maisha yake yalivyo kwa sasa na yupo na faraja kwa kujitambua yeye pamoja na mazingira yaliyomzunguka.

 

Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment