×

Watu 34 Wauawa Katika Shambulizi Lililotokea Shule ya Chekechea

Wanafunzi wa shule ya chekechea nchini Thailand

WATU 34 wameuawa leo katika shambulizi la kutumia bunduki na kisu lililotokea katika shule ya chekechea nchini Thailand.

 

Taarifa inaeleza kuwa shambulizi hilo limetekelezwa na  Afisa wa zamani wa Polisi ambaye alimuua mkewe na mwanae kabla ya kujiua kwa kujipiga risasi.

 

Afisa huyo alifukuzwa kazi mwaka jana na Jeshi la Polisi la nchi ya Thailand kwa sababu zinazohusiana na dawa za kulevya.

Shambulio limesababisha vifo vya watu 34 katika shule ya chekechea nchini Thailand

Afisa wa wilaya Jidapa Boonsom amesema takribani  watoto 30 walikuwepo shuleni hapo wakati mtu huyo aliyekuwa na bunduki alipoingia majira ya mchana na   watoto 22 ni miongoni mwa wahanga wa shambulizi hilo.

 

Polisi wamesema kuwa awali mshukiwa wa mauaji hayo alianza kuwapiga risasi wahudumu takribani watano akiwemo mwalimu ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi nane.

Askari aliyeshukiwa kutekeleza mauaji hayo

Matukio ya ufyatuaji risasi ni nadra sana kutokea nchini Thailand lakini kiwango cha umiliki wa bunduki ni cha hali ya juu ikilinganishwa na nchi nyingine za kanda hiyo.

 

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Prayuth Chan-ocha ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu waliofiwa na kueleza kuwa tukio hilo ni la kushtusha.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment