×

Biden Aitahadharisha Dunia Juu ya Matumizi ya Nyuklia, Adai Putin Hatanii

Rais wa Marekani Joe Biden

RAIS wa Marekani Joe Biden ameitahadharisha dunia ikiwemo Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin hatanii anapoongelea kuhusu suala la matumizi ya nguvu ya nyuklia kutokana na namna ambavyo anazidiwa katika vita dhidi ya Ukraine.

 

Biden amesisitiza kuwa kauli ya Putin ianatakiwa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa kwani majeshi yake yamekuwa hayafanyi kazi sawasawa.

Mabomu ya Nyuklia

“Kwa mara ya kwanza tumekuwa na vitisho vya moja kwa moja vya matumizi ya Nyuklia tangu mgogoro wa makombora wa Cuba. Hatujawahi kutana na uwezekano wa matumizi ya nyuklia tangu enzi za Kennedy.” alisema Rais Biden.

 

Katika hotuba yake ya Ijumaa ya wiki iliyopita Rais wa Urusi Vladimir Putin aliyakumbusha mataifa ya Ulaya Magharibi pamoja na Marekani kuhusu tukio la nyuklia lililotokea Japan.

Vladimir Putin, Rais wa Urusi

Aidha Putin amesisitiza juu ya kutumia kila aina ya mbinu na uwezo wake wote kuilinda mikoa minne iliyochukuliwa na serikali yake kutoka Ukraine, mikoa ya Luhansk, Kherson, Donetsk pamoja na Zaporizhzhia.

Leave a Comment