×

Ten Hag Awawashia Moto Sancho na Malacia, Aoneshwa Kutofurahishwa na Kiwango Chao

Erick Ten Hag akiwa na Tyrell Malacia

KOCHA wa Manchester United Erik Ten Hag amewajia juu wachezaji wake wawili Jadon Sancho pamoja na Tyrell Malacia kutokana na kucheza katika kiwango cha chini wakati klabu hiyo ikiibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Omonia Nicosia katika mechi za kombe la Europa hapo jana.

 

Katika mchezo huo Omonia Nicosia ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kutokana na makosa yaliyofanywa na wachezaji hao wawili kitendo ambacho Ten Hag ameoneshwa kukasirishwa nacho.

 

Ten Hag alitoa kauli tata wakati akijibu swali la mwandishi wa Habari mara baada ya mchezo kumalizika kuhusu uamuzi wake wa kuwatoa Malacia na Sancho kama ulichagizwa na wao kufanya vibaya katika mchezo huo.

Tyrell Malacia

“Siyo kilichonikasirisha lakini upande wetu wa kushoto sikupendezwa nao kwani hakukuwa na mikiombia ya mpira ndiyo maana nikaamua kumuweka Luke Shaw pamoja na Marcus ili tupate matokeo zaidi upande ule na kwa maoni yangu nadhani tulifanikiwa.” alisema Ten Hag.

Jadon Sancho dhidi ya Omonia Nicosia

Manchester United ipo katika nafasi ya pili ya msimamo wa kundi hilo ikiwa na alama 6 nyuma ya Real Sociedad yenye alama 9 huku huku Sheriff ikibaki na alama zake 3 na Omonia Nicosia ikiburuza mkia na alama 0 baada ya kupoteza michezo yote.

Leave a Comment