
Simba SC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Primeiro De Agosto na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla (aggregate) ya 4-1.
Simba SC ilishinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza kule Angola na kumalizika shughuli Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Droo ya Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kupangwa Novemba 2022 ikishirikisha timu 16 zitakazokuwa katika makundi manne na kuchezwa kuanzia Februari 10, 2023.
