×

Simba Wawaka… Chama Ametibua Hesabu za Mgunda Dhidi ya Singida leo

Kiungo wa Simba raia wa Zambia, Clatous Chama (katikati) akifanya yake. Kulia ni Kiungo wa Yanga, Aziz Ki na Kushoto ni Kiungo wa Yanga, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ .

 

UNAAMBIWA kumbe baada ya Bodi ya Ligi Kuu Bara kumpiga rungu la kumstopisha kucheza mechi tatu kiungo wa Simba raia wa Zambia, Clatous Chama, imetibua hesabu za ushindi wa mapema wa kocha Juma Mgunda.

 

Leo Simba itakuwa ugenini Uwanja wa Liti, Singida kupambana na Singida Big Stars kwenye mchezo wa raundi ya 9.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema, rungu la Chama limetibua mipango yao, kwani takribani wiki nzima wamejifua wakijua atakuwa sehemu ya mchezo huo ila sasa kuondolewa kwake kumetibua sehemu kubwa ya mipango ya kocha wake Mgunda.

 

“Naomba nikiri tu wazi kuwa, pengo la Chama kwetu limetibua sana baadhi ya mipango ya makocha wetu kwa maana ya Mgunda na msaidizi wake Seleman Matola, ambapo wamemuandaa kucheza kwa takribani wiki nzima hivyo kutokuwepo kwake kutaleta pengo kubwa.

 

“Chama ni kati ya wachezaji wetu wakubwa na tegemeo, hivyo ni lazima atibue hesabu kwani kwa sasa alikuwa ni mchezaji wa moto sana hivyo kukosekana kwake hatuwezi kusema hatujadhurika kitu, kubwa makocha wetu wataona namna ya kuziba pengo lake ili tuweze kupata ushindi.

 

“Tunatambua tunacheza na Singida ambayo ndani yake kuna wachezaji kama Pascal Wawa na Meddie Kagere, ambao wanatufahamu vizuri hivyo tuko makini sana kuhakikisha tunapata ushinda kwani mbali na wao kutujua hata sisi tunawafahamu vyema hivyo tutatumia mapungufu yao pia kupata ushindi,” alisema Ahmed.

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA WANATOA TAARIFA NDEGE YA PRECISION ILIYOANGUKA KAGERA

Leave a Comment