
12 Desemba 2022: ASKOFU Mkuu Nathaniel Kagwila Mwakibiti wa Kanisa na Growing Mission Church (SMC) With Union For The Gospel Ministries (UGM) ametunukiwa tuzo ya Uzalendo na Taasisi ya Wananchi Wazalendo Tanzania (TWWT) kufuatia mchango wake mkubwa wa masuala ya kizalendo na taifa lake la Tanzania.

Askofu Kagwila alitunukiwa tuzo hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika kanisa lake lililopo Bagamoyo, Pwani nyuma shule ya Baobab na kuhudhuriwa na wageni kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Marekani.

Katika tukio hilo pia kulikuwa na utoaji vyeti kwa watumishi wa Mungu waliokuwa wakisoma kozi kanisani hapo.

Baada ya kupewa cheti hicho mgeni rasmi katika hafla hiyo aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni alisema Askofu Kagwila amestahili tuzo hiyo ya heshima kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwenye taifa hili la Tanzania.
Awali ilielezwa kwenye risala iliyosomwa kanisani hapo kuwa askofu huyo licha ya kuishi nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 35 lakini ameendelea kupakumbuka hapa Tanzania nchi yake aliyozaliwa kwa kuwekeza kwenye mambo mbalimbali.
Miongoni mwa taasisi za kizalendo alizofungua hapa nchini ni pamoja na vituo vya kulelea watoto yatima, makanisa, huduma ya matibabu ya vidonda sugu huduma aliyoifungulia kisiwani Zanzibar nk.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY