Rais Samia: Sijawahi Kuruhusu Utekelezaji wa Adhabu ya Kifo (Picha +Video)
Global Publishers July 13, 2026 18 views 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi, Mawakili, wageni mbalimbali, kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Jijini Arusha tarehe 13 Julai, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema hajawahi kusaini hati ya kuruhusu utekelezaji wa adhabu ya kifo kwa mfungwa yeyote tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania.
Akizungumza leo, Julai 13, 2026, katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali uliofanyika jijini Arusha, Rais Samia alisema moja ya maamuzi mazito anayoweza kuyafanya kama Mkuu wa Nchi ni kuridhia utekelezaji wa adhabu ya kifo, lakini hadi sasa hajawahi kufanya hivyo.
“Kalamu yangu ina mamlaka ya kusaini mtu anyongwe baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika, lakini sijawahi kutumia mamlaka hayo,” alisema Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Bw. Bavoo Anatoly Junus kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Jijini Arusha tarehe 13 Julai, 2026.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 325(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Rais ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kusaini hati ya utekelezaji wa adhabu ya kifo, kubadilisha adhabu hiyo au kutoa msamaha kwa mfungwa aliyepatikana na hatia ya kosa linalostahili hukumu hiyo.
Kauli ya Rais Samia inaendana na mwenendo wa marais waliomtangulia, ambao pia hawakutekeleza adhabu hiyo kwa kusaini hati za kunyongwa. Miongoni mwao ni Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete na Rais wa Awamu ya Tano John Magufuli.
Kauli hiyo imekuja katika mjadala unaoendelea kuhusu matumizi ya adhabu ya kifo nchini, huku hukumu hiyo ikiendelea kuwepo kisheria lakini kutotekelezwa kwa muda mrefu.
Viongozi, wageni mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali wakiwa kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali (TPBA) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Jijini Arusha tarehe 13 Julai, 2026.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kitabu cha Falsafa ya Sheria ya Mama Samia (Mama Samia Doctrine of Law); kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamza Johari kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Jijini Arusha tarehe 13 Julai, 2026. Kitabu hicho kinaelezea historia, falsafa na mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia