×

Jumuia ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam Yapata Safu Viongozi Wake

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Dar es Salaam, Hadija Ally Said akiendesha mkutano huo na uchaguzi mdogo wa kuipata safu yake.

 

Dar es Salaam 14 Desemba 2022: Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Dar es Salaam hatiamaye imepata safu ya viongozi baada ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Hadija Ally Said kuitisha baraza rasmi na kuteua wajumbe wa baraza hilo na wajumbe wa kamati ya utekelezaji kwa ridhaa wajumbe wa baraza la mkoa.

Akizungumza baada ya kukamilisha kuipata safu ya wajumbe wake Mwenyekiti Hadija alisema;

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi wa kukamilisha safu ya Jumuiya ya Wazazi mkoa wa DSM.

 

“Kwasasa safu ya Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam imekamilika ambapo ina wajumbe wa kamati ya utekelezaji wajumbe wa kamati tendaji lakini pia wajumbe wa baraza rasmi.

“Sasa naomba nitoe dira kuwa mkoa wa Dar es Salaam Jumuiya ya Wazazi inakwenda kusimamia mambo yake makuu matano ambayo ni elimu, malezi, afya, mazingira na uchumi katika mkoa wa Dar es Salaam.

Wajumbe ndani ya mkutano huo.

“Jumuiya ya Wazazi CCM inadili na mambo hayo matano na kama mnajua mkoa wa Dar es Salaam mmomonyoko wa maadili umekithiri sana hivyo tunakwenda kudili na hilo na hayo mengineyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata safu yake ya watendaji.

 

“Jumuiya kwa kushirikia na makatibu wetu wa kata zetu zote 102 tutahakikisha tunatoa mafunzo ya uongozi kupitia kamati za utekelezaji na kamati za wilaya.

Mmoja wa wajumbe akiandika barua ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi zilizokuwa zikitangazwa.

 

Jumuiya ya Wazazi inakwenda kuandaa mpango kazi wa miaka mitano kuhakikisha majukumu yake hayo inayafanya kifasaha na kurejesha heshima na hadhi ya jumuiya yetu na kufanyakazi iliyotukuka kuhakikisha chama chetu kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa 24/25″. Alimaliza kusema mwenyekiti huyo. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment