×

Mazishi Ya Winga Christian Atsu Kufanyika Kijeshi… Makamu wa Rais wa Ghana Afunguka

Winga Christian Atsu enzi za uhai wake.

DURU za habari kutoka nchini Ghana zinadai kuwa mazishi ya winga Christian Atsu yanaweza kufanyika kijeshi kama sehemu ya heshima ya taifa hilo kwa winga huyo aliyeifanyia makubwa nchi hiyo kwenye soka.

Mwili wa Atsu, aliyefariki baada ya tetemeko la ardhi kutokea Uturuki wiki mbili zilizopita, umerudishwa nchini kwao Ghana Jumapili iliyopita.

Ndege iliyobeba mwili huo ilitua mjini Accra mwishoni na jeneza lake likabebwa na wanajeshi wa Ghana.

Atsu alipatikana amefariki Jumamosi iliyopita akiwa amebanwa na ukuta nyumbani kwake kusini mwa Uturuki. Alikuwa akiichezea klabu ya Hatayspor.

Winga huyo aliichezea timu ya Taifa ya Ghana mara 65 na kuisaidia timu yake kufika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alichezea klabu za Premier League Everton na Newcastle.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Kotoka katika Mji Mkuu wa Accra, Makamu wa Rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia alisema walisali na kuomba Atsu apatikane na alipopatikana hakuwa hai.

Accra, Ghana

MASHABIKI SIMBA WALIPUKA, WATAJA USHIRIKINA – “HAWASOMEWI DUA, KOCHA AONDOKE HATUMTAKI”….

Leave a Comment