
Mshambuliaji wa Young Africans SC, Fiston Mayele ameshinda tuzo ya Mchezaji bora (MVP) wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2022/23.
Mayele ametwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia klabu yake hiyo kutwaa kombe la Ligi Kuu ya NBC 2022/23 huku akichangia magoli 20 (magoli 17, asisti 3).
Mshambuliaji wa Young Africans SC, Fiston Mayele na kiungo wa Simba SC, Saidi Ntibazonkiza wametwaa tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC 2022/23.
Ntibazonkiza na Mayele wametwaa tuzo hiyo baada ya Kila mmoja kufunga magoli 17 kwenye Ligi kuu ya NBC msimu 2022/23.