
Ni Rasmi sasa, Uongozi wa Yanga umemtangaza Kocha msaidizi ambaye ni Moussa Ndao raia wa Senegal kuchukua nafasi ya Cedrick Kaze ambaye amemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu uliopita.
Utambulisho huo unakuja kujibu swali la Wananchi lililokuwa likiuliza ni nani atakayekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.
Kocha huyo ni Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal na Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kabla ya kwenda kukipiga katika timu ya Al Hilal ya Saudi Arabia ambayo hivi karibuni imenasa saini za wachezaji wakubwa wa soka duniani akiwemo Ruben Neves.

Miongoni mwa timu ambazo kocha huyo amewahi kuzifundisha ni pamoja na Wydad Athletic Club msimu wa 2014 mpaka 2016, Timu ya Sportive Jeanne d’Arc na Sporting Club Chabab Mohammedia.
Aidha, uongozi wa Yanga umemshukuru kocha Msaidizi Cedric Kaze kwa kipindi alichohudumu chote alichohudumu kama kocha msaidizi wa klabu hiyo na kumtakia kila la kheri kwenye safari yake mpya.