×

Namungo Wana Imani Na Cedric Kaze Watamba Kufanya Makubwa

Kocha Cedric Kaze.

UONGOZI wa Namungo FC, umesema wanaendelea na ratiba yao kama kawaida kwa timu hiyo kujiandaa kambini, huku matumaini yao makubwa msimu ujao wa 2023/24 kufanya vizuri chini ya Kocha Cedric Kaze.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mtendaji Mkuu wa Namungo, Omary Kaya, amesema: “Tunaendelea kujipika, tumemuongeza Cedric Kaze katika benchi la ufundi na yeye ndiye tumempa jukumu la kuwa kocha mkuu, kwa hiyo atakuja kuongeza kitu kikubwa ambacho kitatufikisha katika malengo yetu kwa sababu ametokea katika timu kubwa.

“Ukiachana na kuwa mzoefu wa Ligi ya Tanzania, lakini pia timu yetu anaijua vizuri kwa sababu amekuwa akiifuatilia kwa muda wote.”

Kaze ambaye amejiunga na Namungo baada ya kumaliza mkataba ndani ya Yanga alipokuwa kocha msaidizi, atasaidiana na Dennis Kitambi na Shedrack Nsajigwa.

STORI NA AMINA ISSA

#EXCLUSIVE: AUNTY EZEKIEL- “MIMI NDIYE MSANII MWENYE NGOZI NZURI ZAIDI, NDOA KWANGU HAPANA”…

Leave a Comment