×

Mwili Wakutwa na Silaha Bila Kibali Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili Nerbat Mwasile (33) Mkazi wa Ifumbo na Isaya Julias Zumba (38) Mkazi wa Airport Songwe kwa tuhuma ya kupatikana na Silaha bunduki aina ya Shortgun Pump Action bila kuwa na kibali cha umiliki wa silaha hiyo.

Aprili 29, 2023 Usiku huko maeneo ya Nzovwe Jijini Mbeya, watuhumiwa walivunja Jengo la Black Microfinance Bank na kuiiba silaha hiyo.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya ufuatiliaji na mnamo Mei 11, 2024 huko Kijiji cha Itete kilichopo Kata ya Isuto, Mkoani Mbeya lilifanikiwa kumkamata Nerbat akiwa na silaha hiyo.

Aidha, mtuhumiwa alikiri kuitumia silaha hiyo katika matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kushirikiana na mwenzake.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na mahojiano na watuhumiwa hao ili kupata mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na matukio hayo.

Leave a Comment