
Kampuni ya kuunda dawa za kupunguza uzito, Wegovy, imekuwa kampuni yenye thamani zaidi barani Ulayana kuondoa ufalme wa kampuni ya mavazi ya kifahari ya Ufaransa ya LVMH.
Hisaza kampuni hiyo zilipanda baada ya kampuni kubwa ya dawa ya Denmark, Novo Nordisk, kuzindua dawa hiyo maarufu nchini Uingereza.
Mwishoni mwa siku ya Jumatatu, kampuni hiyo ilikuwa na thamani ya soko la hisa ya $428bn (£339bn).
Dawa hiyo sasa inapatikana katika mfumo wa huduma ya afya ya umma wa Uingereza na pia kwenye soko la kibinafsi.
Wegovy ni dawa ya kuzuia unenepaji kupita kiasi ambayo hutumiwa mara moja kwa wiki ambayo ‘huudanganya mwili’ kufikiria kuwa tayari umeshiba, kwa hivyo wanaishia kula chakula kidogo na kupoteza uzito.
Watu mashuhuri kama vile Elon Musk ni miongoni mwa watumiaji walioripotiwa wa kutumia dawa hiyo, ambayo imevutia wasanii wa Hollywood na umma kwa upana zaidi tangu ilipoidhinishwa na wadhibiti nchini Marekani mnamo 2021.
Wegovy na Ozempic -dawa za kisukari zenye athari sawa – zimetajwa kama dawa za “muujiza”.
Lakini wataalam wanaonya kuwa tiba hizo sio suluhisho la haraka wala zinazoweka kuwa mbadala kwa lishe bora na mazoezi.