
DROO ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilisha ambapo vigogo 16 wa Afrika wamebaini wapinzani wao huku Simba na Yanga wakikwepana.
Simba SC imepangwa Kundi B sambamba na Wydad Casablanca ya Morocco, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Jwaneng Galaxy ya Botswana.
Kwa upande wake Yanga SC imepangwa Kundi D sambamba na Mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad inayonolewa na Kocha wa zamani wa Simba SC, Sven Vandenbroeck na Medeama ya Ghana.
KUNDI A:
• Mamelodi Sundowns 🇿🇦
• Pyramids FC 🇪🇬
• TP Mazembe 🇨🇩
• FC Nouadhibou 🇲🇷
KUNDI B:
• Wydad AC 🇲🇦
• Simba SC 🇹🇿
• ASEC Mimosas 🇨🇮
• Jwaneng Galaxy 🇧🇼
KUNDI C:
• ES Tunis 🇹🇳
• Petro Luanda 🇦🇴
• Al Hilal 🇸🇩
• Etoile Sahel 🇹🇳
KUNDI D:
• Al Ahly 🇪🇬
• CR Belouizdad 🇩🇿
• Yanga SC 🇹🇿
• Medeama 🇬🇭