
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amefanya ziara katika makao makuu ya Kampuni wa Serengeti Breweries Limited (SBL) kwa lengo la kuangalia njia za kuwasaidia wakulima wa ndani na fursa za kukuza sekta ya kilimo kwa lengo la kupata malighafi za ndani kwa bei na ubora unaofaa.
Silinde amezungumza na Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kampuni ya Serengeti Breweries Limited, John Wanyancha.