
Chama Cha wamiliki wa vituo binafsi vya afya Tanzania APHTA kimeiomba serikali kupitia upya utaratibu wa malipo ya mifuko ya afya ili kupunguza ucheleweshwaji wa fedha hizo jambo ambalo linasababisha kushindwa kujiendesha Kwa vituo vingi vya afya nchini
Akizungumza katika Mkutano mkuu wa mwaka wa Chama hicho uliofanyika jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Chama Cha APHFTA Dk Egina Makwabe amesema moja ya agenda iliyojadiliwa kwa kina na wanachama wake ni uratibu wa fedha za mifuko ya bima za afya iliyounganishwa na vituo binafsi kuchelewa kwa muda mrefu wa hadi miezi sita jambo linalosababisha kuzolota kwa huduma za afya kwenye vituo hivyo

Tunaiomba serikali kupitia wizara ya afya ishughulikie tatizo la bima za afya ili vituo binafsi viendelee kutoa huduma Bora Kwa wananchi kupitia bima zao- amesema Dk Egina Makwabe.
Katika hatua Nyingine wanachama wa APHFTA wameipongeza serikali ya awamu ya Sita Chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya afya maana ndiyo mhimili wa Taifa la leo na baadae.

APHTA kilianzishwa Kwa lengo la kuwatambua na kuwaunganisha wamiliki wa vituo binafsi vya afya nchini ili kujenga umoja na kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazohusiana na secta hiyo.