×

Tazama Shamrashamra za Mapinduz Zilivyokuwa Zanzibar, Mwinyi Aongoza Sherehe Za Maadhimisho Ya Miaka 60 – (Picha +Video)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika uwanja wa Amaan Januari  12, 2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi ameongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema Miaka 60 ya Mapinduzi ni hatua kubwa katika mshikamano na umoja na kuwasisitiza Watanzania kuendelea kuenzi umoja huo ulioasisiwa na viongozi waliotangulia.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi zilizofanyika uwanja wa Amaan, Mkoa wa Mjini Magharibi Januari 12,  2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akitoa salamu fupi katika Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.

Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushiriki kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi pamoja na shughuli mbalimbali alizopangiwa katika kufanikisha sherehe hizi.

Aidha , Rais Dkt.Mwinyi ametoa shukrani kwa wananchi wote,viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya siasa pamoja na Viongozi wakuu wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao wameshiriki katika Maadhimisho hayo.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akizungumza.

Vilevile katika kufanikisha sherehe hizo amemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Masoud Othman na kuipongeza Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho inayoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdalla kwa kuyaratibu Maadhimisho hayo.

Halikadhalika amewapongeza Makamanda na Wapiganaji wa vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Idara Maalum za SMZ kwa kuonesha hamasa na gwaride la ukakamavu katika sherehe hizo.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame akizungumza katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika uwanja wa Amaan.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ametoa shukrani kwa wageni kutoka nje ya Tanzania wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimaendeleo kwa kushiriki sherehe hizo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya SMZ na SMT waliohudhuria.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni, Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame, Naibu Rais wa Kenya Mhe.Rigathi Gachagua, Waziri Mkuu wa Burundi Mhe.Gervais Ndirakobucha pamoja na Viongozi Wakuu Wastaafu wa Serikali ya SMT na SMZ.

Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua akizungumza katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika uwanja wa Amaan tarehe:12 Januari 2024.
 Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdalla akizungumza katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliohudhuria Sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria Sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria Sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Askari mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipita mbele ya Jukwaa Kuu wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.

 

Leave a Comment